HATMA YA MIGOGORO BAINA YA WAFUGAJI NA WAKULIMA IMO MIKONONI MWAO

Na Ng’wanza Kamata. Bila kuingiliwa na kuchonganishwa na watendaji na viongozi wa serikali na kisiasa wakulima na wafugaji katika maeneo yenye migogoro wanao uwezo wa kupata suluhu ya matatizo yanayowakabili kwa muda mrefu sasa. Aidha ikiwa ardhi yote inayohodhiwa na watu wachache bila hata kuiendeleza ikigawiwa kwa wazalishaji wadogo wadogo ni wazi itasaidia sana kutatua au kupunguza migogoro maeneo ilikokithiri.

WAZEE WAPENDEKEZA KUUNDWE BARAZA LAO

Katika Mkutano wa Hali ya Amani na Utulivu wa Nchi Yetu ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere na Kufanyika kwa siku mbili , tarehe 19 na 20 Mei 2015, katika Ukumbi wa Nyerere Convention Centre Jijini Dar es Salaam, kulifanyika majadiliano ya vikundi. Moja ya kundi lililojadili na kutoa mapendekezo na maazimio yao ni kundi la wazee. Kaatika taarifa ya kundi la wazee ambalo lilikuwa chini ya uenyekiti wa Prof. Issa shivji, yafuatayo yalikuwa mapendekezo yao.

Yes, In My Life Time chazinduliwa

Maneno ya Saida Yahya-Othman siku ya uzinduzi. Wanamapinduzi … siku zote wanajikita kwenye historia – wana jicho la mbali la kuona nyuma, na hivyo kujenga uwezo wa kufanya uchambuzi sahihi wa hali inayotukabili, ili kujipanga vilivyo kuendeleza mapambano. Hili ni la muhimu sana, katika jamii yetu ambamo historia inakuwa kama ukoma, ambamo wanafunzi wa chuo kikuu leo hii hawajui TANU ni nini, ambamo tunafikiri ukombozi wetu utakuja kwa kuwaiga wengine bila ya kuhoji, ambamo tunafikiri utaifa ni chuki dhidi ya waliokuwa tafauti na sisi na uzalendo uchwara.