WAJIBU-JAMII WA MWANAZUONI WA AFRIKA

Issa Shivji. Rai yangu kwenu ni kwamba kuna haja ya kufanya utafiti wa msingi na wa maana katika hali yetu halisi (basic research). Kutokana na tafiti hizo tutaweza kujenga nadharia zitakazotuelekeza na kutuongoza juu ya namna ya kuleta mabadiliko ya maana.

Dhana na Maana ya Bunge Maalum la Katiba

Na Issa Shivji. Kwa sababu zisizoeleweka, katika mchakato wetu wa sasa, dhana na maana ya Bunge Maalum imepotoshwa sana na baadhi ya wasomi na wasemaji. Mheshimiwa Warioba katika hotuba yake aliyotoa katika mkutano wa Tanzania Centre for Democracy amejenga hoja kama ifutavyo.