Mlizingatia maoni ya nani, Jaji Warioba?
Na Mwl. Sabatho Nyamsenda. Sababu zilizotolewa na Warioba kwamba Muungano kwa sura yake ya sasa hauwezi kudumu pia hazina mashiko. Eti kwamba Zanzibar tayari imeshajitangaza kuwa ni nchi, na Wabara wanaionea wivu. Na hapa, Warioba anasema, kuna majawabu mawili: ama Zanzibar ibadili katiba au Tanganyika nayo ijitangazie uhuru kamili.