Buriani Mwalimu Yohana J. Muganyizi: Bingwa wa Hisabati na Fizikia Aliyewajali Watoto Wa Wanyonge

Na Sabatho Nyamsenda: Katika fikra za Mwalimu Muganyizi, ukombozi wa pekee kwa wanyonge wa nchi hii utapatikana kwa kuwapa elimu bora watoto wao. Elimu bora ni zaidi ya kufundisha kanuni za hesabu na fizikia, bali kuwafungua macho wauone uonevu na unyonyaji unaofanywa na watawala, pamoja na kuwaongezea hasira ili wakapambane na unyonyaji huo. Mapambano dhidi ya udhalimu yanaanza katika jamii na taasisi uliyomo.