TANZANIA! TANZANIA

Julius.K.Nyerere. “Niliuliza mwanzoni: Sera hii ni ya nani? Serikali kuwa tatu, Hapa Tanzania kwetu? … Ye yote mwenye akili, Asiyekuwa jahili, Sera hii anajua Itavunja Tanzania.

Buriani Mwalimu Yohana J. Muganyizi: Bingwa wa Hisabati na Fizikia Aliyewajali Watoto Wa Wanyonge

Na Sabatho Nyamsenda: Katika fikra za Mwalimu Muganyizi, ukombozi wa pekee kwa wanyonge wa nchi hii utapatikana kwa kuwapa elimu bora watoto wao. Elimu bora ni zaidi ya kufundisha kanuni za hesabu na fizikia, bali kuwafungua macho wauone uonevu na unyonyaji unaofanywa na watawala, pamoja na kuwaongezea hasira ili wakapambane na unyonyaji huo. Mapambano dhidi ya udhalimu yanaanza katika jamii na taasisi uliyomo.

Dhana na Maana ya Bunge Maalum la Katiba

Na Issa Shivji. Kwa sababu zisizoeleweka, katika mchakato wetu wa sasa, dhana na maana ya Bunge Maalum imepotoshwa sana na baadhi ya wasomi na wasemaji. Mheshimiwa Warioba katika hotuba yake aliyotoa katika mkutano wa Tanzania Centre for Democracy amejenga hoja kama ifutavyo.

Mlizingatia maoni ya nani, Jaji Warioba?

Na Mwl. Sabatho Nyamsenda. Sababu zilizotolewa na Warioba kwamba Muungano kwa sura yake ya sasa hauwezi kudumu pia hazina mashiko. Eti kwamba Zanzibar tayari imeshajitangaza kuwa ni nchi, na Wabara wanaionea wivu. Na hapa, Warioba anasema, kuna majawabu mawili: ama Zanzibar ibadili katiba au Tanganyika nayo ijitangazie uhuru kamili.

Ukimya wa wengi kuhusu muungano: Nini tafsiri yake?

Na Mwl. Sabatho Nyamsenda. Kwa hiyo swali la kujiuliza ni kuwa kama kweli muundo wa Muungano ndiyo kero kuu ya wananchi wetu, Bara na Visiwani, ilikuwaje watoa maoni wapatao 287,537 (sawa na asilimia 86.2 ya watoa maoni wote) hawakugusia kabisa suala la Muungano au muundo wake? Je, kwa nini sauti zitokanazo na ukimya wao zinapuuzwa?