3 thoughts on “SARE SARE

 1. Gabriel niwe mkweli kuwa niliuandika ubeti huu zamani kidogo baada ya kusoma kitabu cha Prof. Mamdani ( Good Muslim, Bad Muslim http://www.amazon.com/Good-Muslim-Bad-America-Terror/dp/0385515375 ). Humo mwandishi anajenga hoja kwamba Marekani na vikundi vya kigaidi ni ‘saresare’ kwa sababu vikundi vingi vya kigaidi ni zao la moja kwa moja au lisilo la moja kwa moja la Washngton yenyewe.
  Ni kweli kwamba kinachoendelea nchini hasa kwenye mchakato wa katiba mpya ndicho kilichonisukuma kuukumbuka ubeti huu. Kama ujuavyo, ushairi kama ilivyo kazi nyingine za fasihi una uwezo mpana wa ku-accomodate tafsiri na uchambuzi wa aina mbalimbali.
  Kwa ujumla, jamii nyingi zina orodha ndefu ya watu ambao wewe unaweza kudhani ni maadui kumbe ukifanya uchambuzi wa kina utagundua kuwa ni ”Sare Sare”

 2. Na kuna mjadala mkubwa sana duniani leo juu ya wimbo wa ugaidi na kuhusisha na masuala ya dini.
  Jambo ambalo tunapaswa kujifunza kwenye historia kwanza ugaidi ni mchakato wa mabeberu katika kutimiza miradi yao ya kujitanua. Maana miradi yao ndio matokeo ya ugaidi. Mfano mzuri tuitizame libya baada ya kusambaratika nini kimetokea?

  pili. Haitoshi kuona vikundi hivi vya kigaidi kama vikundi vya kidini. Lazima twende mbali zaidi na tupekua na kuvielewa kama vyama vingine kwenye demokrasia hii ya kibwanyenye ambavyo navyo vinatafuta maslahi.
  kwa maana kwamba tuvipe alama za kutafuta maslahi yao kwa kutumia mwavuli wa dini.

Leave a Reply to Ado Shaibu Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Please type the characters of this captcha image in the input box

Please type the characters of this captcha image in the input box