Yes, In My Life Time chazinduliwa

Maneno ya Saida Yahya-Othman siku ya uzinduzi. Wanamapinduzi … siku zote wanajikita kwenye historia – wana jicho la mbali la kuona nyuma, na hivyo kujenga uwezo wa kufanya uchambuzi sahihi wa hali inayotukabili, ili kujipanga vilivyo kuendeleza mapambano. Hili ni la muhimu sana, katika jamii yetu ambamo historia inakuwa kama ukoma, ambamo wanafunzi wa chuo kikuu leo hii hawajui TANU ni nini, ambamo tunafikiri ukombozi wetu utakuja kwa kuwaiga wengine bila ya kuhoji, ambamo tunafikiri utaifa ni chuki dhidi ya waliokuwa tafauti na sisi na uzalendo uchwara.